Monday, October 31, 2016

Wazazi pamoja na watoto 476 kufundishwa biashara



Mama mjamzito

WASICHANA 476 mwenye umri kuanzia miaka 11 hadi kufikia 17 waliokuwa katika masomo shule za msingi na sekondari katika Manispaa ya Morogoro na kupata mimba na kushindwa kuendelea na masomo, wamejitokeza kujisajili na Shirika lisilo la kiserikali la Young Strong Mothers Foundation (YSMF) ili kupata


JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA KWENYE MAKWAPA

Hakikisha unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bacteria chini ya makwapa, ambayo husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili. Wakati wa majira ya joto, ambapo ni wakati jasho linakutoka mara kwa mara na husababisha jasho na harufu chini ya kwapa hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku na sabuni antibacterial na maji moto. 

Safisha nguo katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na mafuta, na kuvaa tu mashati safi na undergarments. Inapendekezwa kuvaa mavazi ya maandishi nyuzi za asili, kama vile pamba na hariri, na nyingine kama hizi ili kusaidia kunyonya unyevu na kuruhusu ngozi yako kupumua.
Wakati unafanya mazoezi tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevu mbali na makwapa ili kuzuia harufu mbaya.

Vinega, Witch Hazel na Tea Tree Oil


Apple cider siki, vinega nyeupe na witch hazel kupunguza  harufu kwenye makwapa kwa kupunguza pH kwenye ngozi. Bakteria wanaisababisha harufu kwenye makwapa hawezi kuishi wakati pH wa ngozi ikiwa ni ndogo. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega au witch hazel na kupaka katika makwapa badala ya, au kabla, deodorant. Tea Tree Oil  inaweza pia kuwa na manufaa kutokana na tabia yake ya antibacterial.

Limau

Kata Limao au ndimu nusu kwa kisu chenye ncha kali.Paka kipande cha limau ulichokata kwenye kwapa lao na kahihisha unalissueeze mpaka litoe maji yake.Weka makwapa yako yapate hewa, ili hiyo juice ya limau uliyopaka ikauke. 
 
Asidi citric katika maji ya limau yataneutralize secretions na kutoka tezi ya jasho, na hivyo kuneutralizing harufu.


NJIA 2 ZA KUSAFISHA MENO YAKO YAWE MEUPE.

Meno yanakuwa ya njano kutokana na vyakula & vinywaji tunavyokunywa, na pia inategemea ni vipi unatunza afya yako ya meno, kama unapiga mswaki vizuri, unasafisha vizuri au vipi. Kama meno yako si ya rangi ile inayotakiwa chagua kati ya hizi njia 2 kutumia maramoja kila wiki.

Baking Soda na juice ya ndimu.

Baking soda ina sodium bicarbonate ambayo inasaidia kuondoa madoa na rangi ukichanganya na ile juice ya ndimu inasaidia kupunguza alkaline iliyopo kwenye ndimu.

 Changanya juice ya ndimu pamoja na baking soda kupata paste nzito, futa meno kuondoa mate kisha chukua mswaki wako chota mchanganyiko then paka kwenye meno (usipige nayo mswaki kama unavyotumia dawa ya mswaki, paka tu!), iache kwa dakika 1 then sukutua na maji. Fanya hivi mara moja kwa wiki.

Coconut oil rinse/Tumia mafuta ya nazi.

Tumia mafuta ya nazi kila asubuhi kusukutua kabla hujapiga mswaki. Weka kisi cha kutosha mdomoni then anza kusukutua, zungusha katika kila kona, fanya kama unavuta na kuyasukuma humo mdomoni lakini usiyameze. Fanya hivi kwa dakika 10-15.
Ukishamaliza hivyo sukutua then piga mswaki kama kawaida.

Friday, October 28, 2016

Tumia limao kuondoa madoa meusi usoni



KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.
Ngozi kwa kawaida inatakiwa ijitengeneze yenyewe na si kuitengeneza kwa vipodozi kama wengi wanavyodhani. Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa siku ni njia nzuri kama unataka kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu ambao haupendezi.
Wengi wanaacha kula mbogamboga na matunda kwa wingi hata kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa akitegemea kuwa na ngozi nzuri jambo ambalo ni gumu.Mara kadhaa tumeshuhudia watu wanaopaka cream kali wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili ukionekana kuwa makavu jambo ambalo linaashiria kuwa kupaka cream  si suruhisho la kuwa na ngozi nzuri.
Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili na hata unapowauliza baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado wana ngozi nzuri zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha wanatengeneza ngozi zao kutoka ndani.
Pia wengi wanaharibu ngozi zao na kuwa na madoa kutokana na kutumia make up kwa muda mrefu  na hata anapogundua kuwa ana tatizo la madoa amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo jambo ambali linazidisha madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa usoni  pia mashavuni kwa kujitibu na juisi ya limao.
Namna ya kufanya
Chukua  limao lioshe na kisha likamue na kuchuja mbegu zake. Weka juisi hiyo kwenye kikombe na kisha tafuta kitambaa laini  kichovye kwenye juisi ya limao na dondoshea juisi ya limao kwenye sehemu zenye tatizo.
Kaa  kama dakika tano kisha usha uso kwa maji safi.Pia unaweza kuchanganya na asali mbichi  na maji ya limao husaidia pia kuondoa madoa usoni.
Limao lina sifa kubwa ya kuzuia harufu pia unaweza kulitumia katika kuondoa harufu kali ya jasho mwilini  na husaidia kuondoa weusi kwenye kwapa, chini ya macho, mapajani pia.
Chukua kipande cha limao  weka sukari kidogo, sugua.Unatakiwa kutumia kwenye kwapa ambalo ni safi, vizuri kutumia njia hii kabla na baada ya kuoga.

zijue dondoo muhimu za kutunza kucha zako

Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.

Wanawake wengi na hata Wanaume pia wanaume hupenda kutunza kucha zao, kwani hujikuta wakikutana na vikwazo vya kushindwa kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha zao, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.

Kwanza kabisa ni marufuku mtu kula kucha zake kwani nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu ambao hupenda kula kucha zao, hivyo husababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.

Tumia glovsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele.

Dawa hizi za nywele ni kali sana hivyo huleta madhara makubwa endapo itashikwa bila kizuizi chochote na kusababisha rangi hiyo kushindwa kukaa vizuri.

Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu.

Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu. Kwani watu wengi hupenda kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha zao, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.

Usitoe hovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.

Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa.

Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, baada ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembe au kitu chenye makali.

NA: hadijaty abdallah

Jinsi ya kutumia Asali katika Urembo wa Nywele na Ngozi .

Jinsi ya kutumia Asali katika Ngozi

  
Asali hutumika kulainisha Ngozi
Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.
Jinsi ya kuandaa
 Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.


Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi
Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.

Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator 
Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.

Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung'aa.


Jinsi ya kutumia asali katika nywele

 

Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.  
Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.

pia

Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.

Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.

Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.

Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia.

SERIKALI imesema itaongeza nguvu na kuwawezesha vijana washiriki kikamilifu katika mipango ya kilimo nchini kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuona jinsi ya kuwaondoa vijana katika umasikini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka alisema hayo katika mkutano wa kuhusisha vijana katika kilimo nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema serikali inaweka mipango rafiki kuhakikisha vijana hawapati changamoto nyingi katika kilimo kwa kuwakutanisha pamoja na kuunganisha fursa zilizopo katika kilimo ili kupunguza tatizo la ajira nchini.