Dar es salaam.Naibu
waziri wa michezo wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO),Ally Makame amesema
ataboresha michezo mbalimbali katika chuo hicho baada ya kuporomoka kwa
takribani miaka miwili.
Akizungumza na waandishi wa habari
chuoni hapo,Ally Makame amesema,Chuo cha DSJ hakina muhamko mkubwa katika sekta
ya michezo tofauti na ilivyokuwa miaka mitatu nyuma,Kwasasa kimeshuka katika
sekta hiyo ya michezo kutokana na wanafunzi kukosa morali katika kushiriki
michezo.
Amesema,Ili kuweza kuboresha sekta ya
michezo chuoni hapo,Tayari ameshakutana na makocha wa michezo mbalimbali ili
kuzungumzia na kutatua changamoto hizo za michezo katika chuo cha (DSJ) kwa
lengo la kurudisha ramani ya michezo chuoni hapo.
Pia amesema,Ili kukuza na kuboresha
sekta ya michezo ameutaka uongozi wa juu chuoni hapo kushirikiana na uongozi wa
serikali ya wanafunzi (DASJOSO) ili kuimarisha zaidi sekta hiyo ya michezo
pamoja na sekta nyinginezo chuoni hapo.
‘’Napenda kuwasisitiza wachezaji wa
chuo chetu cha (DSJ) tusisubiri mpaka mechi ndipo tufanye mazoezi kwani jambo
hili litapelekea kushuka kwa sekta ya michezo.”Alisema Makame
Hemedi Fikiri ambaye ni mwanafunzi wa
stashahada ya kwanza chuoni hapo amesema,Anaamini Makame ataimudu sekta ya
michezo chuoni hapo itakayopelekea kuleta mabadiliko makubwa na kuondoa
matabaka yaliyopo katika sekta ya michezo chuoni hapo.
Amesema,Baadhi ya wanamichezo
wameweka matabaka ya urafiki,Ikiwa kupanga timu bila kufuata kanuni na
utaratibu za kimichezo na baadhi yake hupelekea sekta ya michezo kuporomoka
chuoni,Pia amewashauri wachezaji wa chuo cha (DSJ) kuondoa chuki zisizokuwa na
tija ili kuboresha sekta ya michezo.
“Ili kukuza sekta ya michezo chuoni
kwetu lazima wachezaji waondoe chuki zisizokuwa na tija pamoja na kuondoa
matabaka ya urafiki ili kusaidia sekta ya michezo chuoni kwetu.”Alisema Fikiri
Baada ya mchakato wa uteuzi wa baraza
la mawaziri lililoteuliwa mnamo oktoba mosi mwaka huu,Mawaziri walitoa ahadi
mbalimbali za utekelezaji katika majukumu lakini baadhi ya wanafunzi
walisubiria ahadi ya Naibu waziri wa michezo hatasemaje katika sekta yake ya
michezo baada ya kuteuliwa.
Naibu waziri wa michezo wa serikali
ya wanafunzi (DASJOSO),Ally Makame amehaidi kutatua changamoto mbalimbali
katika sekta ya michezo ili kuimarisha hali na nguvu chuoni hapo,Na kutoa
ubaguzi wa kimatabaka katika michezo ili tuweze kufika mbali kama ilivyokuwa
miaka iliyopita.
Uongozi wa juu wa chuo cha uandishi
wa habari Dar-es-salaam (DSJ) umehaidi kushirikiana bega kwa bega katika
kuboresha sekta ya michezo chuoni hapo na kuwaandalia mashindano iliwaweze
kujiweka sawa na kujianda kushindana na vyuo vingine na kuwaongezea vifaa vya
michezo.
Naibu waziri wa michezo amesisitiza kwa wanamichezo
kujitokeza kikamilifu katika kushiriki katika michezo mbalimbali na kujiweka na
maandalizi ya mashindano yatakayokuja siku za usoni na kushiriki katika mechi
za madarasa ilikutafuta timu itakayotuwakilisha.
No comments:
Post a Comment