Na: HADIJA ABDALLAH
Dar
es salaam, Katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi katika chuo
cha uandishi wa habari dar es salaam(DSJ)Angel william amehaidi kuweka usawa wa
kijinsia kati ya wanafunzi wa kike na kiume chuoni hapo,ili kumpa nafasi mtoto
wa kike kwenye sekta mbali mbali chuoni
hapo

Amesema jamii
inapaswa kutambua kitendo cha kumnyima nafasi mtoto wa
kike katika kufanya
maamuzi ni kumnyima haki ya kijinsia,hivyo amewataka wanafuzi wa kike chuoni
hapo kujitokeza kwenye fursa mbali mbali ili kuondoa dhana potofu zilizojengeka
kwa watoto wa kike
Pia amesisitiza kauli
mbiu ya mtoto kike akiwezeshwa
anaweza,Mara nyingi watoto wa kike wanadharauliwa kwa kuonekana hawana kitu
katika jamii kwahiyo amesisitiza kuitumia kauli hiyo ili aweze kuhutumia fursa
hiyo kuweka usawa baina ya mtoto wa kike na
wa kiume katika usawa wa kijinsia.
Aidha,Ameongeza kwa
kusema kuwa uongozi wa serikali yake itawapa kipaumbele watoto wa kike ili
kutoa fursa kubwa ya uongozi chuoni hapo kwani hiyo itapelekea watoto wa kike
kujiamini kwa kila jambo ambalo watakalo lifanyahata pale watakapo maliza
taaluma zao.
“Mtoto wa kike ana
haki sawa na mtoto wa kiume katika kufanya maamuzi mbalimbali ,hivyo jamii
inapaswa kuondoa dhana potofu ya kuwa msichana ni wa kufanya kazi za nyumbani
,kwani fikra hizo zinapaswa kuondolewa, nikiwa katibu mkuu wa serikali ya
wanafunzi(DASJOSO) nahaadi nitawapa kipaumbele katika uongozi.Alisema Willium
Doreen Alex ambaye ni
mwanafunzi wa stashahada ya kwanza chuoni hapo amesema,Amepokea vizuri siku ya
mtoto wa kike duniani anaona kama faraja kubwa kwa maadhimisho ya siku hii ya
leo kwani inamthamini na kumpa nafasi mtoto wa kike.
Amesema ,Kupitia siku
hii atahakikisha anaonesha mfano kwa jamii kuwa msichana anaweza kama mvulana,
endapo atasikilizwa na kupewa nafasi
kwenye sekta mbalimbali kwani hiyo itapelekea kufanya mambo makubwa tofauti na
jamii inavyofikiri.
Aidha,Ameongeza kuwa
serikali ya wanafunzi iwape kipaumbele watoto wa kike katika kuwapa nafasi za
juu za uongozi chuoni hapo ili kuwapa morali na kujiamini katika kufanya
maamuzi mbalimbali.
“Nimefurahi na
nimepokea vizuri siku ya mtoto wa kike duniani nikiwa kama msichana natarajia
kufanya mambo makubwa kwenye sekta mbalimbali ili kuondoa dhana potofu
zilizojengeka katika jamii.”Alisema Alex
Mnamo mwaka 2012
umoja wa mataifa ulitangaza rasmi kuanza kuhadhimishwa kwa siku hii,Hivyo kila
oktoba 11 ni siku ya mtoto wa kike duniani katika kutambua haki zao
mbalimbali.Hivyo kwa Tanzania tunaadhimisha kwa miaka mitatu tangu kudhimishwa
kwake.
Kauli mbiu ya mwaka
huu ni kuwezesha mtoto wa kike katika kufikia malengo ya maendeleo katika jamii
na kumpatia fursa mbalimbali,Ili jamii itambue kuwa mtoto wa kike ana haki kama
mtoto wa kiume.
Katika maadhimisho ya
mtoto wa kike duniani,Katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO) katika
chuo cha uandishi wa habari Dar-es-salaam,Angel Willium ameelezea changamoto
mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike chuoni hapo.
Hata hivyo,Katibu
mkuu wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO) ameahidi kufanya mambo makubwa kwa
watoto wa kike kupitia serikali yake,Ili kuwapa fursa zinazojitokeza katika
chuo cha (DSJ) na ameitaka jamii kuondoa dhana potofu kwa mtoto wa kike
kuonekana hawezi kuongoza kwenye ngazi za juu.
No comments:
Post a Comment