
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka alisema hayo katika mkutano wa kuhusisha vijana katika kilimo nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema serikali inaweka mipango rafiki kuhakikisha vijana hawapati changamoto nyingi katika kilimo kwa kuwakutanisha pamoja na kuunganisha fursa zilizopo katika kilimo ili kupunguza tatizo la ajira nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Charles Tulahi alisema wanaisaidia serikali katika kuandaa sera, mipango, miradi na kutafuta rasilimali katika kutekeleza mpango huo.
Pia wanaendeleza vijana ambao ni nguvu kazi kubwa katika kuendeleza kilimo, kwa kuwa vijana wana changamoto nyingi lakini iwapo wataziondoa wataweza kukuza kilimo.
No comments:
Post a Comment